MKE NA MUME WAUAWA MIILI YAO YAFUKIWA JIKONI.



Na Hadija Omary Mazezele-Tabora

Watu wawili Mke na Mume ambao waliripotiwa kupotea Januari 7 mwaka huu huko katika kijiji cha Nata kata ya Miguha  wilayani Nzega mkoani Tabora wamekutwa wamefariki dunia huku miili yao ikiwa imefukiwa ndani jikoni kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi tukio ambalo linahusishwa na mgogoro wa kifamilia.


Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul matiko Chacha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kikatili huku akifafanua kwamba jeshi la polisi mkoa wa Tabora linawashikilia watu wawili akiwemo kiongozi mmoja wa serikali ya mtaa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya wanandoa hao.


Aidha Paul Chacha amewahakikishia ulinzi na usalama wananchi wa mkoa huo huku akisema serikali itaendelea kuwasaka na kuwakamata wale wote wenye nia ovu.


Kuweza kutazama Video ya maelezo ya mkuu wa mkoa Paul Chacha Bonyeza link hapo chini


https://youtube.com/shorts/ZRiRZtiWKjM?si=_iVyqfGDsET2ETM0

Post a Comment

0 Comments