ALIYEJIFANYA AFISA WA IKULU AKAMATWA KWA UTAPELI.

 




ALIYEJIFANYA AFISA WA IKULU AKAMATWA KWA UTAPELI.

Na Hadija Omary Mazezele Tabora.

Mtu mmoja anayeda­i­wa kuwa raia wa Burundi, aliyekuwa akiishi nchini Kenya, amekamatwa katika mpaka wa Namanga akituhumiwa kujihusisha na jaribio la utapeli katika Kanisa la EAGT Tabora kwa kujifanya afisa wa Ikulu.


Kwa mujibu wa taarifa, mtuhumiwa huyo alidai kiasi cha shilingi milioni 15 akieleza kuwa ni “shukrani” kwa madai ya kusaidia kanisa hilo kupata msaada wa shilingi bilioni mbili kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa anasubiri kupokea fedha hizo.


Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo pia aliwahi kuwasiliana na watu mbalimbali wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, huku akihusishwa na viashiria vya uchochezi wa vurugu.


Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limewaonya wananchi na watu wote wanaojihusisha na vitendo vya utapeli kuacha mara moja, likisisitiza kuwa linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama.

Post a Comment

0 Comments