CHEM CHEM SAFARI & LODGES WAINGIA UBIA NA AUBERGE COLLECTION






Kampuni ya Chem Chem Safari, ya Tanzania imeingia katika ushirikiano na Auberge Collection chini ya chapa ya Auberge Safari.

Ushirikiano huu umejengwa juu ya dhamira ya pamoja ya kutoa huduma zinazozingatia mazingira ya eneo husika, zilizoandaliwa mahsusi na zikizingizatia urithi, utamaduni wa maeneo, na uhusiano na
mazingira hayo.


Uidhinishaji wa Auberge unaongeza alama inayotambulika ya ubora wa kitaalamu
wa bidhaa ambayo imeheshimika kwa muda mrefu katika soko maalum la wateja.

Ikiwa kati ya Ziwa Manyara na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Chem Chem ni chimbuko la falsafa ya “Slow Safari” mtazamo mpya wa uzoefu wa safari unaojengwa juu ya
uzoefu wa makusudi, uwepo wa kweli, na uhusiano wa kina zaidi na mazingira ya asili.

Kila moja ya kambi zake tatu ina sifa ya kipekee: Chem Chem Lodge kama sehemu
ya mapumziko ya kifahari na tulivu; Little Chem Chem ikiibua ukaribu wa kambi ya
mtindo wa wachunguzi (explorer-style) na Forest Chem Chem ikitoa faragha na
uzoefu wa kutulia ndani ya mazingira ya msitu tulivu.

Uhifadhi wa mazingira uko katika msingi wa shughuli zake.

Kupitia Taasisi ya Chem Chem, kampuni inasaidia kulinda Korido/ Njia ya Wanyamapori ya Kwakuchinja, ambayo ni njia muhimu ya uhamaji wa wanyama inayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na hifadhi ya Ziwa Manyara, pamoja na kuendesha programu za maendeleo ya jamii kwa muda mrefu.

Muhimu zaidi, ushirikiano wa Auberge Safari unaimarisha maono haya huku umiliki wa
kampuni na dhamira zake za uhifadhi zikiendelea kubaki bila mabadiliko.

Fahari ya Tanzania, falsafa ya slow safari, na dhamira ya muda mrefu ya Chem Chem
kwa ardhi na jamii vinaendelea kubaki vilevile kama siku zote tofauti ni kwamba sasa
vinawafikia watu wengi zaidi duniani walio tayari kuvitambua.

Kuhusu Chem Chem Safari

Chem Chem Safari ni kampuni ya safari yenye umiliki binafsi iliyoko kaskazini mwa
Tanzania, iliyoanzishwa na Fabia Bausch na Nicolas Negre.


Kambi zake tatu za Chem Chem Lodge, Little Chem Chem na Forest Chem Chem ziko katika eneo la hifadhi ya kipekee kati ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ziwa Manyara.

Chem Chem ni nyumbani kwa falsafa ya “Slow Safari” na inaendesha Chem Chem
Association, inayosimamia shughuli za uhifadhi na programu za jamii katika Ukanda wa Wanyamapori wa Kwakuchinja

Kuhusu Auberge Collection

Auberge Collection ni mkusanyiko wa hoteli 39 za kipekee, risoti, kambi za safari, nyumba za kulala wageni, makazi na vilabu binafsi katika mabara matatu. Kila eneo
lina utofauti wake, lakini yote yanazingatia ubunifu wa hali ya juu, vyakula bora,
ustawi wa kisasa, na huduma ya kiwango cha juu.

Auberge inawaalika wageni kutengeneza kumbukumbu zisizosahaulika katika maeneo yanayotamaniwa zaidi duniani.

Kwa maelezo Zaidi tembelea:

Post a Comment

0 Comments