MISA TAN YASISITIZA HABARI ZA MAENDELEO NA WELEDI KATIKA UANDISHI WA HABARI



Na Hadija Omari Mazezele

MWANZA

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania (MISA Tanzania), Edwin Soko, amevitaka vyombo vya habari nchini kuendelea kuandika na kuripoti habari zenye kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku vikizingatia weledi, ukweli na taarifa zilizohakikiwa.


Soko ameyasema hayo wakati wa Kongamano la MISA TAN Wadau tarehe 12 oktoba, 2026 lililofanyika jijini Mwanza, likiwa na kaulimbiu ya “Uhuru wa Vyombo vya Habari Kiuchumi”, lililowakutanisha wanachama 60 wa MISA Tanzania kutoka Kanda ya Ziwa inayojumuisha Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara na Kagera ,Kanda ya Magharibi Kigoma, Tabora na Katavi,na Kanda ya Kati  inayojumuisha Singida na Dodoma.pamoja na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na sekta binafsi.


Amesisitiza kuwa waandishi wa habari wana wajibu mkubwa wa kuelimisha jamii na kuchangia maendeleo kupitia habari zenye tija, huku akiwataka kuzingatia maadili ya taaluma, kufanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha taarifa wanazochapisha au kurusha zimethibitishwa ili kuepusha upotoshaji na uchonganishi katika jamii.


Aidha, Soko amesema MISA Tanzania inatambua umuhimu wa ushirikiano kati ya vyombo vya habari na wadau kutoka sekta mbalimbali, akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuimarisha tasnia ya habari na kuwezesha vyombo vya habari kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.


Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali, zikiwemo Idara ya Uhamiaji, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), pamoja na taasisi nyingine.


Hata hivyo kongamano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango kazi wa mwaka wa taasisi hiyo, likilenga kuwakutanisha wanachama na wadau kwa ajili ya kujadili masuala ya uchumi wa sekta ya habari na maendeleo ya Tanzania.









Post a Comment

0 Comments